Sponsor scroller

Redds

VODACOM


AIR TANZANIA

DSTV

http://wwww.dstv.com

NBC and The OTHER

Adsense and Twitter

TUFUTA KITU BLOGUNI HAPA

Loading...

JACKZ COSMETICS

CLASSIC COSMETICS

ZHONGHUA GARDEN SOCIAL HALL

MAFIAN FISH LOUNGE

MATANGAZO......KONG'OLI BANNER UONE BIDHAA

KIDAKA POCHI - ZINAPATIKANA ..... 8020 FASHIONS

Thursday, February 23, 2012

UJUMBE


katika kuelekea kilele cha siku ya mwanamke duniani na katika jitihada mbali mbali za kumsaidia mwanamke, pia kutokana na sababu zangu binafsi ambapo nina dhamira kuu 2. kwanza ni kumsaidia mwanamke mwenzangu na pili ni kuonesha shukuran yangu kwa mungu kwa alichonibariki ambapo nami nitapata kuwapa faraja wanawake wenzangu, nimeamua kuanzisha blog inayoitwa www.mwanamkenauzazi.blogspot.com

blog hii inalenga kumuelimisha mwanamke kuhusu mambo yote ya uzazi hasa kwa wale wanaochelewa kupata kizazi au kukosa kabisa (infertility) . blog hii pia inalengo la kuwapa moyo wale wote wenye matatizo hayo lakini pia kuelimisha jamii na umma uache kuwanyanyapaa wale wenye matatizo. humu pia tutajadili masuala mbali mbali yanayohusiana na uzazi, na pia wadau watapata nafasi ya kutoa maoni yao.

Mwanamke ana shida nyingi kimaisha ila asilimia kubwa ambayo jamii huipa msukumo ni shida za kiuchumi na shida hii ya uzazi imesahaulika na kufikia hatua mpaka kumuona mkosaji ni yeye mwenye tatizo la hilo na pia huliona kama ni tatizo lake binafsi, wanafamilia na jamii haliwahusu, wakati tatizo hili ni kubwa, linawaathiri wengi na linahitaji msaada wa kipekee sio pesa wala nyumba ambavyo vinaweza kumsaidia. Naongea hayo kutokana na uzoefu kwani hata mimi nilipita huko. Hivyo basi naomba msaada wa kushare na jamii  blog hii ili lengo litimie na tuweze kumkomboa mwanamke huyu. Tushirikiane kumsaidia mwanamke na pamoja tutashinda.

1 Maoni:

Anonymous said...

dear shamim
nashukuru sana kwa hii post imesaidia sana hadi napata faraja moyoni, u are an angel my dia na mungu atakulipa kwa wema wako. kila mwanamke akifanikiwa na kushukuru mungu basi na wewe upo nyuma yake. nakuombea kwa mungu ufanikiwe kwa kila unalolifanya. nitakutumia email tuwasiliane zaidi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...