SPONSORED BY MERCY G BEAUTY PARLOUR

NEW ARRIVALS 8020 FASHIONS

Wednesday, May 30, 2007

KIPO JUU!!

Huu mguu ndo upo juu kwa sasa usake plzz!!...coz unawakilisha Bongo mpaka New York. ipo katika rangi tofauti mbele ipo kama konzi hivi kisigino cha nyumba ni chakumwaga, ukikutana na kinene usistukeee....HII NDO INAREPLACE WEDGE???!!
Beyonce nae anacho!!

Jlo nae anavyooo!!

Friday, May 25, 2007

FASHION POLICE!!

Kumchisha sio issue now days.....ni top dress na leggings
Na mie nilihudhuria Kill Award...pembeni model wangu Dinna ..ni mambo ya 8020 hayo .....ahsante Father Kidevu kwa Picha www.blog.co.tz/mrocky
Kijani hutilia mwilini.......
Kaka Michuzi aliwakilisha ni alikuwa FULL white...kama chamilion lol.. nimependa nguo ya Hafsa hili ni bazee hili ina limetupiwa na kitambaa chenye rangi za TZ kweli huu ubunifu :Picha ahsante Kaka Michuzi
Kumbe nywele zina nguvu.....Nancy aliamua kutoka na natural...enzi tunasoma tulikuwa tunaita kijinja!!:picha ahsante Kaka Michuzi Kanga ikipangiliwa hutulia.... hakika amependeza picha:Kaka Michuzi


That Ray to thee C baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya mwimbaji bora wakike...Kivazi matata..uyoga style
Maimarth wa Jesse akiwakilisha na Tibaigana style na top dress
Nilizimikia huu mguu kama kuna hereni hapo

...Nimependa style ya kofia..hata pozi
the same as here...kofia na pozi...top na hereni make up ndo usiseme
ni mmechisho kwa kwenda mbele
pozi...kapri..top ...jewellers...kiatu

Mambo ya kiafrika yakimixiwa na kizungu huwa hivi!!......THANKS Jestina
Top dress...leggings...the pouse...kacute!!
Hair style...top..so Classic..Neema umeshatua Bongo

Hurrey thats my Girl...Handbag chata gani iyoo...white with red ni taamu
I love the shoe...na rangi ya kucha
Hujagundua ana Tibaigana...Leggings...Top ....Apple Green...Handbag.
I love the shoes Most
Mambo ya vivazi vya usiku..Hellow Wa mjini kasoro bahari
Picha nyingi ahsante hi5...Lol

Thursday, May 24, 2007

KWA WATARAJIWA

Mamboo mashost nimepata maombi kadhaa yakiniomba niwasukumie mavazi ya harusi wedding dress...nimejaribu kusaka fashion za kisasa na nimejaribu kuonyesha old fashions
KUHUSU RANGI YA MWAKA ESPECIALLY KWENYE MAHARUSI.....KWA KWELI BADO SIJAPATE JIBU KAMILI LABDA MWENYE UJUZI NAZO ATUANDIKIE ila mie napenda apple Green, baby Blue, Hellow!! i love this style...huyu ni bi Harusi Lady Jay Dee aliamua kutoka na style ya pekee

Mh hii plz its too old fashion....Usiifikirie kabisa na hili joto letu la bongo ndo kabisa labda waulayaaa
Kama hii imetulia mshono wa juu lakini hiyo mshono wa chini..aka sijapenda
Hii nimependa kuanzia juu na ilivyobana...hata huku chini tausi style sio mbaya...BUT.....
Woa ningekuwa mie i'll go for this simpla and classic

Huyu nae mshono wachini ni wa bibi harusi wa ZAMANI .....Cinderela style...ila kapendeza
...LOL....no comment nasubiria kutoka kwenu.....
Hiii sio mbaya lakini ataevaa awe mreefu au avae viatu virefu ili hiyo style ya chini ionekane....mshono wa mikono hii wanashona kwa wale kanisani ambao hawa

Tuesday, May 22, 2007

BRAZIA NA NAFASI YAKE

Haya mashost leo nimegeukia upande huu, wa mambo ya LINGERIE....hususan kipande cha juu hiki BRAZIA...wengine wazitambua kama SIDIRIA....
Sio siri nakaraishwa kuona mdada na sidiria inamning'inia mikanda iko nje katika nguo ambayo sidiria haitakiwi kuonekana
na ndio maana kuna sidiria hizi ambazo zina mikanda ya blastik yote nikatika kuficha sidiria isionekane, au la kama nguo yako transparent vaa na sidiria nyeusi au vaa sare na rangi ya blouzi......na kama we una boops na wataka zionyesha..zipo sidiria zake....kodolea chini picha utazitambua Mikanda ya maji hiyo vaa iwapo maziwa mazito, yanahitaji suport kwa nguo isiyo na mikono au wazi

Vaa hii kama nguo yako iko wazi nyuma backless

Una boops wewe....vaa hii
Hii vaa na half top ambayo haina mikono
hii vaa na back less...kama huna mdoa ka kenge...lol
boops na uhakikishe inabeba mzigo wa matiti fresh...kama maziwa mazito itaharibu mambo


hii vaa na kivazi chochote hususan cha material kama t-shirt...flat

Monday, May 21, 2007

Dont...Usijaribu!
















Hata siku moja warembo wenzangu usijari na wala usisubutu kuvaa au kumatch mavazi namna hii kwakuwa utaonekana kituko ile mbaya na watu watakushangaaaaa.Embu tazameni walivyochemsha mhhh hii hatari..au mnasemaje warembo wenzangu hii kweli saw walivyovaa?

Friday, May 18, 2007

WEEK END NITOKE VP?!!!

Aaaaa NDO MAANA YAKE JAMANI CHEKI HAO MACELEBRATE WA ULAYA WAMELIPUKAA...haya mashost peruzini peruzini mtaweza kupata tipu WEEK END MTOKE VP




Wednesday, May 16, 2007

MAMBO YA 8020FASHIONS!!

Ni yule yule Model wangu Dinna akiwa ametinga top ...mkanda na viatu toka duka la 8020fashions

Monday, May 14, 2007

NDIO MAANA YAKE SHERIA!!

kwenye blog ya swahiba wangu....SHERIA ....nimekutana na hiki kivazi cha TRASSPARENT!! .. Akihoji bado zipo???...NAMI NAMJIBU KWA MSISITIZO ZIPO NA ZINARUDI KWA KASI......huyo ASHANT kajilipia na maroon, KLYN wa bongo ye alilipuka na black...Hii ilikuwa ni kwenye show ya Hassanali...enjoy...... MIND YOU....ukivaa kivazi hicho zingatia unachokionyesha kiwe una uhakika nacho.....sio mikovu....minyama uzembe. K LYN.....ndani ya strasparent na skin jeans!!

ASHANT....ndani ya trassparent...Picha shavu kutoka kwa Sheria...mzee wa Pamba

Friday, May 11, 2007

LOW CUT JEANS NAZO KWAHERI!!

sio siri kipindi cha kati hapo zilipoingia low cut jeans...nilikuwa nahangaika saana kupata jeans ya kunitosha hataka kama nikifanikiwa ikaniingia ila itabidi nitembee na skafu ya kufungaa maana ilikuwa ukikaa huko nyuma...SHANGA NJE.....lol

hebu cheki hizi Low cut jeans sasa umkute mdada mwenye makalio ya haja atakaa kweli kwenye siti ya daladala....ehe ziishie tu kwa kweli tumechoka ona chupi...lol
Duh bora ziende at last nasi mabonge nyanya wenye shape za kibantu ..... wo! wo! wo!...tutapata size na jeans na tuvae tuenjoy

Furaha yangu ni kurudi kwa hii fashion ya mabwanga ambapo na suruali zinaanzia kiuno na sio zile JLO style

Mind u:-JAPO HIZI SURUALI KWA WALE VIPOTABLE ITABIDI WAFIKIRIE MARA MBILI KABLA YA KUVAA MAANA WENGINE ZINAWAFANYA KITUKO

Thursday, May 10, 2007

TUMPIGIE KURA FLAVIANA MATATA

NI MWAKILISHI WETU WA MISS UNIVERSE YUPO MEXICO KWA SASA


KUMPIGIA KURA KONGOLI HAPA, KISHA CLICK VOTE NOW....UMUWEKE FLAVIANA NAMBA MOJA NAWENGINEO HADI 11...KISHA TUMA...KILA SIKU INARUHUSIWA KUVOTE

Tuesday, May 08, 2007

THIS WAS TIGO MAMA AFRIKA!!...ilinoga

NI ILE FASHION SHOW YA MUSTAFA HASSANALI!!! ILIKUWA BOMBA KULIWAKUWA NA JEWELLERS ZA SHANGA ZILIZOPEWA JINA LA SHANGALICIOUS....NGUO KIBAO....SIZE TOFAUTI HADI BIG MAMA'S.... KUNA MAVAZI HAYO NAWAOMBA KINA DADA WENYE SEND OFF, KITCHEN PARTY MUMUONE MUSTAFA MIE HADI NILITAMANI NIRENEW YAKWANGU...LOL

SHANGALICIOUS zilionyeshwa kwa mtindo huu!!......LOL hadi za kiuno zilikuwepo....ila za nje si ndani.
HAYA haya ndo mavazi ya mtoko. sherehe especial kwa Bi Harusi kwenye kitchen Part au send off....




Big mama waliwakilishwa na Mc ZIMPOPA POMPA...4 BY 4


kulikuwa na vivazi vya kiofisi pia




Thursday, May 03, 2007

SIMPLE BUT GORGEOUS

Jamani kwa uelewa wangu mdogo nilio nao mie....ukienda shopping au kwenye mizunguko ya week end inatakiwa utoke simpleee... kwa kutinga vgauni (MOCHA DRESS). VIKAPTURA WALE WENYE 'MIGUU YENU'...... na sandoz...FLIP fLOP za kiushkaji aaaa una puyanga kwa raha zako na hata ukivaa jeans poa mradi juu uvae kitu simple...sio top na bling bling nyyingi......MIND U depend on material ya hizo gauni plz


WOW!! my favorite...mi nazimia hutu tusandols ...very confotable.....







Mwepesiii



Lady B yupo around Mazeeeee!!


BILA KUSAHAU HAYO MAGAUNI ......SANDALS...flip flop ZINAPATIKANA 8020FASHIONS sinzaaa.....thoooo SAME SAME BUT DIFFERENT...lol

BLACK WITH RED INATOKA BOMBA

Huku bongo kwetu...ukivaa full black lazima watu watakupa pole ya msiba..... ila kwa sasa ulimwenguni kote ndo mapigo unalipuka full Black inagusia na uwekundu kama dada hapo chini....aaaa UNATOKEA WA UKWEEELI!!!!
BY THE WAY, WHAT IS THE COLOUR OF THE YEAR.......WADAU HEBU TUIJADILI RANGI YA MWAKA PLZ

Wednesday, May 02, 2007

CLUTCHES IN FASHION

Aaaa wanasema baada ya mchana kutwa kushinda umebeba pochi kuuubwa kama lile langu...ucku katika mitoko yako unashauriwa kubeba CLUTCHES...ni aina ya pochi Ndogo ambalo hubebwa mkononi....kwa sasa katika kuliweka katika fashion wameliongeza ukubwa ili liweze kubeba vitu vingi zaaidi.
We siku nzima ushinde umebebeshana na mizigo.....mashost najua mnaelewa usiku unaambiwa beba walet ya pesa na make up ndogo kwa watumiaji kina sie tunabebaga Lipshine tu na perfumNaomba nikukumbushe hizi zinabeba kwenye mitoko ya usiku jamani kama harusi nk..... HOPE MNAMKUMBUKA my sis sophy so zinaenda saana na evening dress...ukikutwa nayo mchana watakucheka watu...ila wala inategemea mwaya uko maeneo gani kama picha hii hapa chini
Blog Widget by LinkWithin